Creating opportunities. Improving lives. Strengthening communities. info@zmbf.or.tz   |   ☎ +255 710 709 205
Education

ZMBF and Mixx na Yas Business wasaini Hati ya Makubaliano (MoU)

image

Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF), Mixx na Yas Business tumesaini Hati ya Makubaliano (MoU) ya kimkakati inayolenga kutumia huduma za kidijitali kunufaisha wakulima wa mwani Zanzibar, hususan wanawake na vijana wanaoshiriki katika programu ya Seaweed Socio-Enterprise.

Makubaliano hayo yametiliwa saini na wakuu wa taasisi zote tatu, Bi. Rehema Tukai, Afisa Mtendaji Mkuu, ZMBF; Bi. Angelica Pesha, Afisa Mtendaji Mkuu, Mixx; na Bw. Norman Kiondo, Afisa Mkuu, Yas Business, katika hafla iliyofanyika Zanzibar na kushuhudiwa na Waziri wa Mawasiliano, Teknolojia ya Habari na Ubunifu Zanzibar, Mhe. Mudrik Ramadhan Soraga.

Ushirikiano huu unatokana na dhamira ya pamoja ya kutumia teknolojia kurahisisha malipo, kuongeza upatikanaji wa huduma za kifedha na kufungua fursa zaidi za kiuchumi kwa wananchi. Kupitia makubaliano haya, Mixx itawezesha wakulima wa mwani kupokea malipo yao kidijitali kwa usalama, uwazi na kasi zaidi, huku wakipata fursa ya kunufaika na huduma kama Kilimo Pesa na Mixx Kikoba za kuweka akiba, kupata mitaji na kukuza shughuli zao.

Mbali na sekta ya mwani, ushirikiano huu pia utasaidia utekelezaji wa programu nyingine za ZMBF ikiwemo Mariam Mwinyi Walkathon na Afya Bora Medical Camps, kwa kutumia mifumo ya kidijitali katika usajili, malipo na uchangishaji wa fedha.

Hatua hii inalenga kuhakikisha kuwa juhudi za maendeleo zinakuwa na tija zaidi kwa jamii, huku zikiwafungulia wananchi, hususan wakulima wa mwani, njia rahisi ya kujikwamua kiuchumi.

More Stories, ideas & impact.

Visit our news centre ↗
Seaweed and blue economy programme
Education

ZMBF and Mixx na Yas Business wasaini Hati ya Makubaliano (MoU)

Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF), Mixx na Yas Business tumesaini Hati ya M...

Read More →
Seaweed and blue economy programme
Seaweed

Visit to seaweed farming

The CEO of Zanzibar Maisha Bora Foundation, Ms. Rehema Tukai, had the honor of l...

Read More →
Seaweed and blue economy programme
Institutional

CEO Meet Mr. Masanori Kobayashi

Our CEO, Ms. Rehema Tukai, had the pleasure of welcoming Mr. Masanori Kobayashi,...

Read More →

We use cookies to enhance your browsing experience, serve personalized ads or content, and analyze our traffic. By clicking "Accept", you consent to our use of cookies. fdd learn more

Allow